Kipa wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Mwadini Ally, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Mwadini aliyeanza kuitumikia Azam FC tokea mwaka 2011 akitokea Mafunzo ya Zanzibar, amesaini mkataba huo rasmi leo mchana,mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na Mratibu wa timu, Phillip Alando.
Habari ambayo imetumwa kwenye akaunti rasmi ya Azam FC imeeleza kuwa mchezaji huyo ameongeza idadi ya wachezaji wa Azam FC ambao wameongeza mkataba wengine wakiwa ni mabeki David Mwantika, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri na mshambuliaji Donald Ngoma.
Uongozi wa Azam FC chini ya Popat kwa kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo, umesema kuwa wanaendelea na zoezi la kuwabakisha wachezaji waliomaliza mkataba pamoja na usajili wa wachezaji wapya wa kuongeza nguvu kikosini kwa ajili ya msimu ujao.