SELEMAN Matola amepewa kandarasi ya kuinoa timu ya Polisi Tanzania iliyopanda Daraja msimu huu kushiriki Ligi Kuu Bara.
Matola ambaye alikuwa kocha wa Lipuli ametambulishwa leo wa ajili ya kuanza kuinoa timu hiyo na atafanya kazi kwa kushirikiana na Ali Suleiman ambaye ndiye mkurugenzi wa benchi la ufundi.
Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa huo ni mwanzo tu kwani mipango ya kikosi ipo sawa kwa ajili ya ushindani.