Home Uncategorized KABLA HAJATUA SIMBA, BWALYA ALIAMSHA DUDE

KABLA HAJATUA SIMBA, BWALYA ALIAMSHA DUDE


MSHAMBULIAJI Mzambia, Walter Bwalya ambaye anatarajiwa kutua Simba siku chache zijazo amechambuliwa kuwa ni mmoja wa washambuliaji wazuri na mwenye uwezo mkubwa wa kufunga mabao uwanjani.

Bwalya ambaye amekuwa akitajwa mara kadhaa, aliwahi kuhusishwa kutua Simba tangu msimu uliopita wakati Simba ilipokutana na Nkana Rangers katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini usajili huo ulikwama.

Beki wa Nkana Rangers, Hassan Kessy ambaye anacheza timu moja na Bwalya, amemzungumzia straika huyo na kudai kuwa ni straika wa kiwango cha juu huku akimtaja beki wa Yanga, Kelvin Yondani pindi Simba na Yanga zitakapokutana na mshambuliaji huyo akiwa uwanjani.

Kessy, ambaye ni beki wa zamani wa Simba, alitua Nkana msimu uliopita akitokea Yanga baada ya mkataba wake kumalizika amefafanua kuwa anamjua vizuri Bwalya kwa kuwa ni mtu ambaye anaishi naye na kucheza naye kuanzia mazoezini hadi katika mechi ngazi ya klabu.

Ifahamike kuwa Bwalya na Simba wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na wakati wowote atatua nchini kwa ajili ya kuja kusaini mkataba wa kukipiga katika timu hiyo, ambapo Msimbazi wanaimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao hasa kuelekea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kessy ambaye yupo kambini na Taifa Stars alisema kuwa kama Simba watafanikiwa kuinasa saini ya Bwalya, basi watakuwa wamefanya bonge la usajili kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao ndani na nje ya 18 kwa kupiga mashuti makali akitumia miguu yote.

Kessy alisema kuwa, pia mshambuliaji huyo ana uwezo wa kufunga kwa kichwa, hivyo anahitaji Wilbert Molandi, Dar es Salaam uangalizi wa karibu kwa maana ya kucheza naye karibu na beki anayestahili kumdhibiti Yanga ni mkongwe Yondani.

Aliongeza kuwa, Bwalya akikabidhiwa Yondani basi shughuli itakuwa kubwa kutokana na uzoefu alionao beki huyo ambaye amekutana na washambuliaji wengi wakubwa.

“Nipo naye huku (Yondani) na tayari nimeshammegea sifa za Bwalya, kuwa jamaa anajua na hatari kwa kupasia nyavu, hivyo ana kibarua kigumu mara watakapokutana.

“Sina hofu na Yondani katika kumdhibiti Bwalya, kwani ni kati ya mabeki bora hivi sasa katika ligi ya hapo nyumbani, ninaamini ushindani mkubwa utakuwepo.

“Bwalya kama akipata wachezeshaji wazuri katika kumtengenezea nafasi za kufunga, basi hao akina Kagere (Meddie) watasubiri, Zambia wapo wachezaji wengi wenye uwezo kama wake wanaotamani kuja kucheza ligi ya Bongo,” alisema Kessy

SOMA NA HII  ZAHERA ASHINDWE MWENYEWE TU