Uncategorized

ALLIANCE FC WAMCHUNIA MALALE HAMSINI

admin June 18, 2019 10:01 am

KOCHA wa Alliance FC, Malale Hamsini amesema kuwa tayari amemaliza mkataba wake ndani ya kikosi hicho hivyo kwa sasa yupo huru kujiunga na kikosi kingine kwa kuwa bado hajaitwa mezani.

Akizungumza na Salehe Jembe, Hamsini amesema kuwa kwa sasa hayupo na timu ya Alliance baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

“Nimemaliza mkataba wangu na Alliance hivyo bado sijaongeza mkataba mwingine kwa sasa, sijazungumza na uongozi wa Alliance kuhusu kuongeza mkataba wangu hivyo bado nipo huru,” amesema.

Malale ameiongoza Alliance kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 11 baada ya kucheza jumla ya mechi 38 ikiwa na pointi 47.

MAKOSA YA MSIMU ULIOPITA YAIPA SOMO SINGIDA UNITED BREAKING: BEKI MWILI JUMBA AMLIZANA NA SIMBA LEO MIAKA MIWILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply