Home Uncategorized MANCHESTER UNITED WAMTAKA KIUNGO WA WESTHAM UNITED

MANCHESTER UNITED WAMTAKA KIUNGO WA WESTHAM UNITED

 MANCHESTER UNITED imewasiliana na uongozi wa West Ham United kuona namna gani wanaweza wakakamilisha dili la kumpata mchezaji Declan Rice.

United wameonyesha uhitaji mkubwa wa kumpata kiungo huyo wa West Ham baada ya kufanya vizuri ndani ya Premier League.

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kujenga kikosi upya na ana mipango ya kuwahi kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao.

WestHam hawana tatizo na kiungo huyo, hesabu zao wapewe Euro milioni 80 wamuachie mchezaji huyo ajiunge na United.

SOMA NA HII  MESSI ATAJA KILICHOMVURUGA NDANI YA BARCELONA