Winga wa klabu ya Lipuli Fc yenye makazi yake mjini Iringa, Miraj Athumani, huenda anaelekea katika klabu ya Simba Sc baada ya kupost picha yake leo akiwa pembeni ya bango la Simba Sc.
Miraji aka Sheva, mfungaji wa mabao 7 msimu uliopita alikuwemo katika kikosi ha wachezaji 32 kilichoenda Misri. Alichujwa katika awamu ya mwisho kupata kikosi cha wachezaji 23.
Winga huyo amewahi kuchezea timu ya vijana ya Simba sc hapo kabla, na amekuwa nguzo muhimu katika kampeni ya Ligi Kuu msimu uliopita kwa upande wa Lipuli Fc.
Tunaendelea kufuatilia zaidiā¦.
The post Miraji avunja kanuni ya saa saba kamili? appeared first on Kandanda.