UONGOZI wa Simba umesema kuwa bado una imani na mchezaji wao wa zamani, Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye ametemwa ndani ya kikosi cha Azam FC kilicho chini ya Etiene Ndayiragije.
Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa ni wakati sahihi kwa Messi kutulia kabla ya kufanya maamuzi.
“Bado ni mchezaji mwenye akili nyingi, uwezo wake hasa wa kutumia mguu wa kushoto na maamuzi ya haraka, hivyo ni muda sahihi kutulia kabla ya kurejea kwenye ubora licha ya kuachwa na Azam FC,” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.