Home Uncategorized VIDEO: ALIYEUA MWANAFUNZI WA KIU AKAMATWA NA POLISI

VIDEO: ALIYEUA MWANAFUNZI WA KIU AKAMATWA NA POLISI


JESHI  la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata Ernest Joseph (19) kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Anifa Mgaya,  aliyefariki dunia Juni 17 baada ya kuchomwa kisu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jumatano Juni 19, Kamanda wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa usiku wa kuamkia leo maeneo ya Madale.

“Mtuhumiwa katika mahojiano na Jeshi la Polisi amekiri kumchoma kisu kilichosababisha kifo cha mwanafunzi huyo huku akieleza namna mwanafunzi huyo alivyokuwa amevaa siku hiyo ya tukio kuwa ni fulana nyeusi, suruali ya ‘jeans’ na kapelo nyeusi.

“Aidha mtuhumiwa alikiri kumpora pochi iliyokuwa na simu moja aina ya Tecno rangi nyeusi, fedha taslimu Shilingi 8,000 na vitambulisho mbalimbali ambavyo alivitupa na simu hiyo kuiuza,”  amesema Kamanda Mambosasa.

Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.


SOMA NA HII  MUONEKANO WA GAZETI LA SPOTI XTRA KATIKA UKURASA WA MBELE LEO ALHAMIS