MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameahidi kutoa eneo la hekari 15 kwa shirikisho la soka nchini (TFF) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha soka.
Makonda ameyasema hayo wakati wa harambee ya kuichangia Taifa Stars iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambako aliwaonya watu wanaohoji viwanja hivyo amevipataje.
Hata hivyo, alisema yeye anapambana kuwaomba watu wenye hivyo viwanja ambapo wamempatia na yeye anavitoa kwa wahitaji ambao ni Yanga na Taifa Stars na wengine ambao watajitokeza kuvihitaji.
”Kuna watu wengine wanahisi mafanikio ya Taifa Stars anayepata heshima Makonda, wengine wanapambana usiku na mchana kupromote watu waonekane ni wa maana zaidi kuliko kazi ya Makonda, kazi yangu ukifahamu wewe, Rais Magufuli na Mungu inatosha.
“Juzi nilitoa ahadi ya kuwapa uwanja ndugu zangu wa Yanga, kesho naenda kuwakabidhi heka zao saba ili waanze ujenzi wa Academy kubwa.
Sina pesa mfukoni lakini Mungu amenipa kibali cha kukubalika na hili jambo watu wengi linawaumiza roho” alisema Makonda.
Kwa habari zaidi sikiliza video ifuatayo chini.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.