Baada ya ukimya wa muda mrefu, hatimaye leo uongozi wa klabu ya Yanga umetoa msimamo wake kuhusiana na kiungo Ibrahim Ajibu Migomba.
Yanga imesema mkataba wake na Ajibu unaisha mwishoni mwa mwezi huu. Tayari wamemka Ajibu nafasi ya kuamua kama atasajili au la.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema tayari wameamuambia Ajibu kama anataka kubaki wanamhitaji lakini kama anataka kuondoka, wanamtakia kila la kheri.
“Tumemueleza nia yetu, kama anataka kubaki tunamsubiri kwa ajili ya kusaini lakini kama anataka kuondoka, basi tunamtakia kila la kheri,” alisema.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwamba tayari Ajibu ameshamalizana na Simba ambayo ni timu yake ya zamani.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.