Home Uncategorized AZAM FC WAIKOMALIA KAGAME, SASA NGUVU ZAO WAMEWEKEZA HUKU

AZAM FC WAIKOMALIA KAGAME, SASA NGUVU ZAO WAMEWEKEZA HUKU

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kwa sasa hesabu kubwa ni kukiandaa kikosi cha ushindani kitakachofanya vema kwenye michuano ya Kagame inayotarajiwa kuanza mwezi Julai nchini Rwanda.

Azam FC ni mabingwa watetezi walitwaa ubingwa kwa kuifunga Simba mabao 2-1 uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Salehe Jembe, Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa mpango mkubwa ni kuwa na kikosi imara kitakacholeta ushindani kwenye michuano watakayoshiriki.

“Tuna kazi kubwa ya kutetea ubingwa wa kombe la Kagame hivyo ni lazima kikosi kijipange na kijiweke sawa kwa ajili ya michuano hiyo ambayo sisi ni mabingwa watetezi,” amesema.


Kwa kuanza Azam FC wameongeza nguvu ya kiungo mshambuliaji, Idd Suleiman kutoka Mbeya City ambaye msimu wa 2018-19 alitupia mabao 10.

SOMA NA HII  KIUNGO RAYON AWAAGA MASHABIKI RWANDA SASA KUIBUKIA YANGA,NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU