Home Uncategorized SIMBA YATOA DOZI JIJINI MWANZA, YAITANDIKA GWAMBINA 4-2

SIMBA YATOA DOZI JIJINI MWANZA, YAITANDIKA GWAMBINA 4-2


Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-2 yaliyopatikana kwa njia ya penati dhidi ya Gwambina FC jijini Mwanza.


Ushindi huo umepatikana kufuatia dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1 katika dakika 90 za mchezo.

Walikuwa ni Gwambina FC walioanza kupata bao lao dakika ya 49 ya mchezo kupitia kwa Anuar Jabir mnamo dakika ya 49.

Bao hilo lilidumu hadi dakika ya 85 kwa Simba kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Said Ndemla kupitia mpira wa adhabu.

Baada ya dakika 90 kumalizika, Mwamuzi aliamuru zipigwe penati ili kumpata mshindi na Simba wakafanikiwa kuingiza kambani mipira minne huku Gwambina wakiweka miwili.

Mechi hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya uzinduzi wa Uwanja huo ambao unatumiwa na Gwambina FC iliyo Ligi Daraja la Kwanza.
SOMA NA HII  DAH! KUMBE AZAM FC NDIO WAMEPANIA NAMNA HII....