Mabingwa wa soka Tanzania, Simba wameongeza nguvu katika safu yao ya ushambulizi baada ya kumsajili, Wilker Henrique da Silva kutoka nchini Brazil.
Wilker amejiunga na mabingwa hao akitokea nchini Brazil.
Uongozi wa Simba umesema umesaini mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji huyo.
Maana yake Mbrazil huyo anaungana na John Bocco, Meddy Kagere na wengine kuimarisha safu ya ushambulizi ya mabingwa hao.
Simba imepania kufanya vizuri Afrika na kuiska mbali zaidi katika ligi ya mabingwa.
Msimu uliopita, Simba ilifika katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuifanya Tanzania kuongeza timu mbili za michuano ya Caf, upande wa klabu.