NAHODHA wa Kenya, Victor Wanyama amewaonya wale wote wanaozibeza Harambee Stars na timu ya Taifa ya Tanzania katika kundi la Tatu la michuano ya CAN inayotaraji kuanza kutimua vumbi lake usiku wa Leo kwa wenyeji Misri kuwavaa Zimbabwe katika mchezo wa Kundi la Kwanza.
Kenya itacheza na Algeria usiku wa Jumapili hii, ikiwa ni muda mfupi baada ya Stars kucheza na Senegal katika mchezo mwingine wa kundi C.
“ Watu wanatutazama Kenya na Tanzania kama ‘underdogs, lakini hawapaswi kusahau kuwa siku hizi nchi nyingi zimebadilika na zimepiga hatua nyingi.” Anasema kiungo huyo wa Tottenham ya England alipozungumza na chombo kimoja cha habari nchini Kenya.
Wakati Tanzania wakitumia ‘msemo’ wa ‘NI ZAMU YETU’ , Harambee Stars wao wanatumia ‘TUNAWEZA’ na timu hizo mbili za Afrika Mashariki zitakutana zenyewe kwa zenyewe Juni 27 katika michezo ya pili kwa kila timu za kundi hilo.
“ Hatujali vile timu nyingine zinavyotutazama, kama vile ilivyo soka, tutawaheshimu wapinzani wet una tunaamini haitakuwa michuano rahisi kwa kila timu.” Anamaliza kusema Wanyama. Kenya, Tanzania, Senegal na Algeria zimepangwa katika kundi moja .
The post Wanyama; ‘Wanasema Kenya na Tanzania ndio underdogs!, tumebadilika appeared first on Kandanda.