Home Uncategorized MO AZUIA JARIBIO YANGA

MO AZUIA JARIBIO YANGA


HELA inaongea nyie! Mwekezaji Mkuu wa Simba bilionea, Mohammed Dewji, amezuia jaribio la kiungo wake mkabaji, Said Ndemla la kwenda kusaini kwa watani wao wa jadi, Yanga.

Hiyo, ikiwa ni siku chache kabla ya kiungo huyo kwenda kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gwambina FC kwenye Uwanja wa Gwambina uliopo Misungwi, Mwanza.

Kiungo huyo hivi karibuni ilikuwa inaelezwa kuwepo kwenye mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kumsajili kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, kiungo huyo hivi karibuni aliitwa ofisini kwa bilionea huyo na kufanya mazungumzo naye na kikubwa ni kutaka kumbakisha Simba.

“Ndemla anabaki Simba na haendi huko Yanga kama inavyoelezwa, kwani wakati wowote atasaini mkataba wa kuendelea kubaki kuichezea Simba.

“Mo alimuita ofisini kwake na kumalizana kwa asilimia kubwa na upo uwezekano baada ya kurejea kutoka Gwambina, basi atasaini mkataba.

“Hivyo, kama Yanga wanamtaka basi hawataweza kumpata tena Ndemla, ataendelea kubaki Simba licha ya kukalia benchi muda mwingi,” alisema mtoa taarifa.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori kuzungumza hilo alisema kuwa: “Sitaki kuzungumza na Waandishi wa Championi, nyie jana (juzi) mlitufukuza na gari lenu hadi Polisi ‘Sentro’ sijui mlikuwa mnataka nini.”

SOMA NA HII  MAKOSA YA MSIMU ULIOPITA YAIPA SOMO SINGIDA UNITED