Home Uncategorized SAMATTA: TUKO FITI, SENEGAL ANAKUFA

SAMATTA: TUKO FITI, SENEGAL ANAKUFA


HAINA kuremba kesho aisee, kwani Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta wamejipanga kuhakikisha wanashinda mechi yao ya kwanza mbele ya Senegal.

Stars kesho itacheza kwa mara ya kwanza michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) baada ya kupita takribani miaka 39 ambapo itapambana na Senegal kwenye Uwanja wa 30 June huko nchini Misri.

Samatta amezungumza na Championi Jumamosi moja kwa moja kutoka Misri ambapo alisema kuwa, licha ya kuamini kuwa mchezo huo utakuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa wao wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanapambana kupata ushindi.

“Jambo kubwa kwa Watanzania wenzangu ni dua zao ili Mwenyezi Mungu aweze kutujalia nguvu za kuhakikisha tunapambana kwa dakika zote 90 ili tuweze kupata ushindi. “Kuhusiana na maandalizi, tumejiandaa vizuri na kila mmoja wetu ana morali ya juu kwa ajili ya mchezo huo,” alisema Samatta.

SOMA NA HII  ARSENAL WASHINDA KIBABE MBELE YA BURNLEY, YAJIPIGIA VIDUDE VIWILI