Kiungo Mapinduzi Balama amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na klabu ya Yanga.
Kiungo huyo amefikia makuabliano na Yanga akitokea Alliance FC ya Mwanza.
Usajili huo unaendelea ikiwa ni moja ya maboresho yanayofanywa na uongozi wa klabu ili kujiandaa kuelekea msimu ujao.
Ikumbukwe kwa Mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela, alisema kuwa wanafanyia kazi ripoti ya Kocha Mkuu Mwinyi Zahera ambaye yuko Misri.
Zahera yuko na kikosi cha timu ya taifa ya Congo akiwa kama Kocha Msaizidi.