Home Uncategorized YANGA YATOA TAMKO JUU YA MBRAZIL WA SIMBA

YANGA YATOA TAMKO JUU YA MBRAZIL WA SIMBA


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa auhofii usajili unaoendelea kufanywa na watani wao wa jadi, Simba ukiwemo wa straika Mbrazili, Wilker Henrique da Silva.

Wiki iliyopita Simba ilimtangaza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo.

Yanga upande wake imefanikisha usajili wa wachezaji kumi kati ya hao sita ni wa kimataifa na watatu wazawa ambao ni Abdulaziz Makame, Mapinduzi Balama na Ally Ally. Kutoka nje ya nchini ni Issa Bigirimana ‘Walcott’, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob, Maybin Kalengo, Juma Balinya, Lamine Moro na Suleyman Mustapha.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliwataka watani wao Simba kuendelea kusajili Wabrazili akiamini ni wa kiwango cha kawaida kama walivyokuwa Wabrazili waliocheza Yanga, Andrey Coutihno, Genilson Santana Santos ‘Jaja’ na Emerson De Oliveira Neves Rouqe.

Mwakalebela alisema wao usajili wao wanaoendelea kuufanya utaendana na ligi ambayo inachezwa kwenye viwanja vibovu kabla ya kwenda kushiriki michuano ya kimataifa, mwaka huu kwa kusajili wachezaji wa ndani na nje ya nchi wenye uwezo na uzoefu ili kuhakikisha wanafikia malengo yao.

Aliongeza kuwa wamepanga kufanya usajili mmoja mkubwa wa kishindo utakaofunga usajili wao kabla ya kuingia kambini kujiandaa na msimu mpya ambao wamepanga kurejesha heshima yao iliyopotea.

“Hakuna Mbrazili atakayekuja hapa nchini mwenye uwezo mkubwa wa kucheza ligi na kufikia hatua ya sisi Yanga kumuogopa, hivyo wakae wakifahamu hatuwaogopi tusubirie ligi ianze.

“Mbrazil anayekuja hapa ni wa kiwango cha kawaida, Wabrazili wa juu ni wale wanaokwenda kucheza ligi ya ushindani Ulaya na siyo hapa nchini ambayo miundombinu yenyewe ya viwanja ni vibovu.

“Hivyo, basi kama Wanayanga wasiogopeshwe na usajili huo unaofanywa na watani wao Simba, kikubwa wasubirie burudani katika msimu ujao kutokana na usajili mkubwa unaoendelea kufanywa na viongozi wao,” alisema Mwakalebela.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: MSIMU HUU USHINDANI NI MKUBWA