Home Uncategorized TBL YAZINDUA KAMPENI YA FRIJI YA USHINDI

TBL YAZINDUA KAMPENI YA FRIJI YA USHINDI


KAMPUNI ya Bia Nchini kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Primium Lager  imezindu Kampeni ya Friji ya Ushindi kwa wadau wote wa soka ili kuhamasisha Watanzania kuishangilia Tanzania  ishinde iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Bar ya Juliana Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Primium Lager, Pamela Kikuli alisema hii ni Kampeni maalumu kwa wadau wote wa soka ili kuweka uzalendo mbele kama Watanzania kuishangilia timu yao na Tanzania ikishinda friji inafunguliwa na kugawiwa bia za Kilimanjaro Primium Lager bure kabisa.

Alisema Kikuli Tbl kuitia Bia yake ya Kilimanjaro wanaamini Watanzania wakiweka uzalendo mbele ni lazima tutashinda hivyo ni wakati maalumu kwetu watanzania tushikamane na lazima tutafika mbali.


Kampeni hii tumeweka friji ya ushindi sehemu mbalimbali ambazo tutataja hapo baadaezikiwa zimejaa bia na Watanzania tukishinda friji ya ushindi inafunguliwa na kugawa bia za Kilimanjaro bure.

Kikuli alisema TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro wakao tayari kutoa hamasa kwa Watanzania wadau wa soka kuungana nao kila Tanzania inavyofanya vizuri kwenye soka.


SOMA NA HII  ISHU YA NIDHAMU YA MORRISON NDANI YA SIMBA IPO HIVI