Home Uncategorized STARS YAENDELEA KUKALIA MKIA KUNDI C AFCON, YACHAPWA 3-2 NA KENYA

STARS YAENDELEA KUKALIA MKIA KUNDI C AFCON, YACHAPWA 3-2 NA KENYA


Kikosi cha Taifa Stars kimpoteza tena mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika awamu hii dhidi ya Kenya kwa kuchapwa mabao 3-2.

Kipigo hiki kimekuwa cha pili baada ya mechi ya kwanza kufungwa mabao 2-0 na Senegal.

Mabao ya Kenya yamefungwa na Michael Olunga aliyeingia kambani mara mbili huku moja likiwekwa kambani na Johanna Omolo.

Wakati Stars imefunga mabao yake kupitia kwa Mbwana Samatta na Simon Msuva.

Stars sasa itakabiliwa na kibarua kingine dhidi ya Algeria Jumatatu kunako kundi C ambapo mpaka sasa haina alama hata moja.

SOMA NA HII  TRENT ALEXNDER WA LIVERPOOL NJE KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND