Ramadhani Singano ‘Messi’ kwa sasa ana ofa kutoka timu tano tofauti ambazo zinaitaka saini yake ili aweze kuzitumikia kwa sasa.
Messi ni mchezaji huru baada ya kutemwa na Azam FC hali iliyotoa nafasi kwa timu hizo ambazo zinahitaji saini yake huku KMC, Polisi Tanzania na Lipuli zikitajwa kuwania saini yake.
Akizungumza na Saleh Jembe, Messi amesema kuwa kwa sasa ni muda wake wa kutulia hivyo mashabiki wasiwe na presha juu ya uwezo wake kwani anajua kazi yake ni mpira.
“Kwa sasa nipo nje ya Dar ila nina ofa zaidi ya timu tano zinahitaji kupata saini yangu, muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi kwani mazungumzo bado yanaendelea,” amesema Messi.