Home Uncategorized PIERRE AUBAMEYANG AIVURUGA ARSENAL

PIERRE AUBAMEYANG AIVURUGA ARSENAL


PIERRE Aubameyang mshambuliaji wa Arsenal amezua taharuki baada ya kusema kwamba yupo tayari kutua Manchester United msimu ujao.

Aubameyang amekuwa akihusishwa kujiunga na United ili akazibe pengo la mshambuliaji Romelo Lukaku ambaye inadaiwa anataka kujiunga na Inter Milan.

Arsenal inamtegemea kwa kiasi kikubwa nyota huyo ukizingatia kwamba ni mfungaji bora kwa msimu wa 2018/19 akiungana na Sadio Mane na Mohamed Salah ambao walipachika mabao 22.

SOMA NA HII  NAMNA MORRISON NA MOLINGA WALIVYOWAFUNIKA WOTE BONGO - VIDEO