Msanii wa Bongo Fleva, Tundaman ambaye alikua golikipa wa Timu ya Bongo Fleva ambayo ilishuka dimbani kuminyana na Global FC nje kidogo ya Jijini la Dar es Salaam, Kibaha na Bongo Fleva kuibuka na ushindi wa matuta kwa mabao 5-3 amefunguka siri ya ushindi huo.
Tundaman amesema kwanza kudaka penalti ni kawaida yake na walipofikia kwenye hatua hiyo alijiweka kudaka penalti tatu hakufanikiwa na kufanikiwa kuzuia penalti mbili na hatimaye kuipa ubingwa Timu yake. Mechi ya kirafiki ambayo imechezwa katika uwanja wa Vikawe huko Kibaha.
SOMA NA HII MO WA SIMBA AKUBALI USAJILI WA YANGA, MORRISON ATUMA UJUMBE, NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU