Home Uncategorized JKT TANZANIA YAMALIZANA NA NYOTA WAKALI SITA FASTA

JKT TANZANIA YAMALIZANA NA NYOTA WAKALI SITA FASTA



DANNY Lyanga amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kujiunga na kikosi cha JKT Tanzania baada ya kuachwa na Azam FC na kukamilisha jumla ya wachezaji sita waliopigwa pini na JKT Tanzania.


Lyanga ameungana na wachezaji wengine watano waliosajiliwa na JKT Tanzania ambao ni pamoja na Jabiri Aziz ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja akitokea African Lyon, Hafidhi Mussa ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ametokea Stand United.

Mshambuliaji Adam Adam kutoka Tanzania Prisons amesaini kandarasi ya mwaka mmoja, Adeyum Saleh kutoka Coastal Union amesaini kandarasi ya mwaka mmoja na Hassan Mwaterema amesaini kandarasi ya mwaka mmoja.
SOMA NA HII  MBELGIJI WA YANGA AKOSESHWA USINGIZI NA MTIBWA SUGAR