Home Uncategorized YANGA YAKAMILISHA ASILIMIA 90 YA USAJILI WA ZAHERA,

YANGA YAKAMILISHA ASILIMIA 90 YA USAJILI WA ZAHERA,


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa umekamilisha mchakato wa usajili wa wachezaji wake kwa asilimia 90 kutokana na maagizo ya kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.

Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla amesema kuwa usajili wote walioufanya umetegema ripoti ya kocha hivyo wana imani wataleta ushindani kwenye michuano ya kimataifa.

“Kazi ya usajili tumeifanya kwa kuzingatia matakwa ya kocha, imani yetu tutafanya kweli kwenye michuano ya ndani na ya kimataifa,” amesema Msolla.

Mashine mpya ambazo zimesajiliwa ni pamoja na Patrick Sibomana, Lamine Moro, Issa Bigirimana, Maybin Kalego, Mustapha Suleiman, Juma Balinya, Sadney Urikhob na Abdulaziz Makame.

SOMA NA HII  ANGUKO LA YANGA DHIDI YA IHEFU WA KULAUMIWA HUYU HAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here