Home Uncategorized HAWA HAPA NYOTA 15 KIMEELEWEKA NDANI YA SIMBA

HAWA HAPA NYOTA 15 KIMEELEWEKA NDANI YA SIMBA

BADO vuguvugu la kuongeza majembe mapya na kuongeza mkataba wa wachezaji kwenye Ligi Kuu Bara unazidi kushika kasi.

Mabingwa watetezi Simba kama ilivyo ada nao hawapo nyuma ambapo mpaka sasa tayari wamemalizana na wachezaji 15.

Hawa hapa mambo safi ndani ya Simba kwa sasa:-

Meddie Kagere mshambuliaji wa Simba na mfungaji bora kwa msimu wa mwaka 2018-19 akiwa ametupia jumla ya mabao 23, ameongeza mkataba wa miaka miwili.

John Bocco, nahodha wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili, msimu wa 2018-19 ametupia jumla ya mabao 14.

Erasto Nyoni, beki kiraka wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili.

Aishi Manula, Mlinda mlango wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka mitatu.

Jonas Mkude, Kiungo wa Simba, ameongezewa mkataba wa miaka miwili.

Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ameongeza kandarasi ya miaka miwili.

Shomari Kapombe beki kiraka wa Simba ameongezewa kandarasi ya miaka miwili.


Clatous Chama, ameongeza kandarasi ya miaka miwili.

Sharaf Eldin Shoboub Ali Abdalrahman, kiungo raia wa Sudan amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ametokea timu ya Al Hilal ya Sudan.

Wilker Henrique da Silva raia wa Brazil amesaini kandarasi ya miaka miwili ametokea Bragantino.


Gerson Fraga Veira ametokea ATK FC ya India yeye ni raia wa Brazil amesaini kandarasi ya miaka miwili.


Beki Tairone Santos da Silva raia wa Brazil amesaini kandarasi ya miaka miwili ametokea timu ya Atletico Cearense FC ya Brazil.

Beno Kakolanya, Mlinda mlango wa Simba amesajiliwa akiwa huru baada ya kuachana na Yanga.


Igizo jipya jingine ni Kenedy Juma ambaye ni beki amesajili akitokea Singida United kwa kandarasi ya miaka miwili naye alikuwa ni mchezaji huru.

Miraji Athuman, yeye ni mshambuliaji amesaini kandarasi ya miaka miwili akitokea Lipuli FC.
SOMA NA HII  MAURICIO POCHETTINO KUIBUKIA PSG