Home Uncategorized MAMA KANUMBA: BABA KANUMBA ALIKUWA MCHEPUKO WANGU TU! – VIDEO

MAMA KANUMBA: BABA KANUMBA ALIKUWA MCHEPUKO WANGU TU! – VIDEO


MAMA wa aliyekuwa staa wa Bongo Movie, marehemu Steven Kanumba, Bi. Flora Mtegoa, amesema hakuwahi kuolewa na baba wa mtoto wake huyo (mzee Charles Kanumba) badala yake alikuwa mchepuko wake tu kwani tayari baba huyo alikuwa na mkewe na watoto.

Bi. Flora amesema hayo jana Jumatatu wakati akipiga stori ndani ya kipindi cha Kata Mbuga cha +255 Global Radio na kusema kuwa mzee huyo hakuwahi kuwa na mawasiliano wala kumhudumia mtoto huyo mpaka umauti ulipomfika, lakini Baba Kanumba amekuwa msitari wa mbele kudai mali za marehemu Kanumba jambo ambalo mama huyo amepingana nalo vikali.

“Huwa nina-miss vingi sana kutoka kwa mwanangu, uwepo wake, upendo wake, waliojifanya ni marafiki zake leo wala huwaoni. Naishukuru serikali baada ya miaka saba ya kifo chake, mikataba ya Kanumba na mzee Majuto imerudiwa. Nilikuwa nalia nikikuta muvi za mwanangu zikichezwa. Namshukuru Rais Magufuli na Waziri wa Sanaa, Dkt. Mwakyembe wamenifuta machozi.

“Nilikuwa sitegemei kupata chochote kutoka kwenye muvi za Kanumba, nilichopewa na Steps (Entertainment) nasema asante na bado niko nao bega kwa bega, tunafanya vitu vingi, siwadai wala hawaniadi.

Kuhusu Baba Kanumba

“Baba Kanumba hajawahi kuja kwenye msiba wa Kanumba, mwanangu alipokufa walimtumia tiketi ya ndege, wakamtumia gari kutoka kwake Shinyanga mpaka Mwanza Airport, hakuwahi kuja, mpaka leo hajawahi kuja, lakini anaposikia kuna pesa anataka kuja, sasa ana uhakika kama Kanumba alikufa?

“Inawezekana sio baba mzazi wa Kanumba, kwa sababu tangu Kanumba alipokuja Dar, hakuwahi kuja kumtembelea wala kujua anaishi wapi, hata kuwasiliana naye, sasa anasubiri kwenye faida, hili nasema liwe fundisho kwa akina baba wanotelekeza watoto.

“Kwa bahati mbaya sikuwahi kuwa na mawasiliano naye, nimekaa Shinyanga miaka 22, Kanumba amesoma pale Shinyanga lakini baba huyu hakuwahi kuwasiliana naye. Akahamia Dar es Salaam, hakuna mawasiliano naye, mpaka amekufa hadi leo hajui hata kaburi lake lilipo.

“Kanumba aliwahi kukaa kwa baba yake kwa miezi tisa, alipotoka huko hakutaka kurudi tena kule. Mzee huyu hakuwahi kunisaidia kwa chochote na nilimwambia apige hesabu ya pesa zake alizowahi kumsaidia huyo mtoto, kama ikifika hata jero namrudishia.

“Mimi nilikuwa mchepuko, sikuwa mke wake, hata mawifi zangu sikuwahi kuwajua, alikuwa na mke wake, na watoto wake. Kwa hiyo aliponipa ujauzito akaiacha, labda alimuogopa mkewe, na mimi kwa sababu nilikuwa nimetoka kuachana na mume wangu wa ndoa, nikasema ndo wanaume walewale. Shinyanga nafahamika kama mama Kajumulo.

“Kanumba hakuwahi kufahamika kwenye familia, hakuwahi kulipiwa mahali ili ahalalishwe kwenye ukoo kama yeye ni Msukuma kwa mila za Kisukuma, wala hakuwahi kuitwa kwenye familia. Kanumba ndo alimtafuta baba wala sio baba alimtafuta Kanumba,” alisisitiza mama huyo.

SOMA NA HII  STARS KUWAKOSA WATATU, HESABU ZAO NI KUSHINDA LEO KWA TUNISIA