Home Uncategorized MSUVA NA SAMATTA WATUMA UJUMBE MZITO KWA WATANZANIA

MSUVA NA SAMATTA WATUMA UJUMBE MZITO KWA WATANZANIA


NAHODHA wa timu ya taifa, Taifa Star,  Mbwana Samatta na mchezaji mwenzake, Simon Msuva,  kupitia kurasa zao za Instagram,  wameandika ujumbe kuwaomba Watanzania radhi kutokana na vipigo walivyovipata nchini Misri katika fainali za mashindano ya ubingwa wa mataifa ya Afrika (Afcon) yanayoendelea nchini Misri.

Katika mchuano huo, timu hiyo ilianza kwa kupoteza  dhidi ya Senegal 2-0,  kisha Kenya 3-2 na mchezo wa juzi dhidi ya Algeria 3-0.

Alichosema Mbwana Samatta: ”Ilikuwa ni ndoto ya kila mtanzania kuona tunashiriki michuano ya #AFCON na sote tulifurahia kupata nafasi hii. Tunafahamu watanzania walitamani timu ifanye vizuri na kufika mbali, hata sisi wachezaji hilo lilikuwa lengo letu namba moja lakini hali halisi imefuta ndoto zetu.

Tunawashukuru mashabiki wote mliotuunga mkono katika kipindi chote kuanzia maandalizi hadi leo, nawaomba mfahamu tu kuwa hili lilikuwa darasa tosha kwetu sote. Ulikuwa ni wakati wa kila mmoja wetu kwa nafasi yake kujifunza kitu.

Alichosema Simon Msuva:  ”Habari zenu watanzania kwa ujumla poleni na majukumu ya kujenga taifa. Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru watu wote waliokuwa wanatusapoti na kutuombea toka tulipoanza mpaka hapa tulipofika,haikuwa kazi rahisi ila juhudi zetu na zenu kwenye maombi. Pia napenda kuwaomba radhi watanzania wote niliowakwaza namna moja Ama nyengine nawaomba muendelee kutuamini na kutuombea. Tulipotoka ni mbali lazima tushukuru tulipo.pia nitoe pongezi na shukurani zangu za dhati kwa wanahabari wote viongozi na wachezaji wengangu kwa kushilikiana vema mpaka tulipofika. Asanteni sana msichoke tukuombea na kuwa nasi katka nyakati zote🙏

SOMA NA HII  YAO NA SOMO KWA WAZAWA MAMBO YAPO HIVI