Home Uncategorized AZAM FC: TUNAPAMBANA KWA AJILI YA TAIFA KAGAME

AZAM FC: TUNAPAMBANA KWA AJILI YA TAIFA KAGAME


KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wachezaji watapambana kupata matokeo chanya kwenye michezo yote ili kurejea na kombe lao la Kagame.


Azam kwa sasa ipo nchini Rwanda ambapo imekwenda kushiriki michuano ya Kagame na kesho itashusha kete yake ya kwanza kwa kumenyana na Mukura.

“Mchezo wetu wa kwanza ni kesho dhidi ya Mukura, hatuwatambui wapinzani wetu ila tunaingia uwanjani kupambana na tunatambua kwamba tunapeperusha Bendera ya Taifa, ni wakati wetu kuonyesha kwamba tumekuja kufanya kweli,” amesema Cheche.

SOMA NA HII  RASMI BOSI SIMBA AANZA KAZI YANGA