Habari za Michezo
Uncategorized

JULIO ATOA TAMKO JUU YA AJIBU KUREJEA SIMBA

admin July 8, 2019 11:32 am


BAADA ya Ibrahimu Ajibu kusaini Simba, aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Jamhuri kihwelo ‘Julio’, amefunguka kuwa hakuna atakayemuweka benchi mchezaji huyo ndani ya Simba.

Julio kwa sasa amepumzika kufundisha soka baada ya kuachana na timu ya Dodoma FC iliyokuwa ikishiriki daraja la kwanza ambayo kwake ilikuwa ya mwisho kuifundisha.

Julio alisema kuwa Ajibu amefanya uamuzi ambao kwake umekuwa ni sahihi, hivyo kutokana na kipaji alichobarikiwa na akijituma zaidi, basi hakuna atakayemuweka benchi Simba.

“Ajibu ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa sana hapa nchini na maamuzi aliyoyachukua kwenda Simba ni mazuri kwa mtazamo wake na kwa kuwa ana uwezo mkubwa na akiongeza juhudi basi hakuna atakayemuweka benchi katika kikosi cha Simba,” alisema Julio.

Ajibu Jumatano alijiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga ambako alicheza misimu miwili ya ligi kuu.

MAJEMBE MAPYA YANGA YAFICHWA HOTELI YA KISHUA KAHATA AANZA NA MIKWARA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply