Mshambuliaji wa zamani wa Simba na baadaye Aza FC, Ramadhan Singano, amejiunga na TP Mazembe ya Congo.
Singano ambaye aliwahi kung’ara zaidi wakati akiwa Simba na baadaye kutimkia Azam FC, amefikia makubaliano na miamba hao wa Afrika kwa kuingia nao mkataba.
Singano amemwaga wino Mazembe akiwa na bosi wa klabu hiyo, Moise Katumbi na sasa atakuwa na kikosi hicho msimu ujao wa ligi.
Mchezaji huyo ambaye alibatizwa jina la Messi wakati akiichezea Simba alishindwana na Azam juu ya mkataba mpya baada ya msimu huu kumalizika.