Uncategorized

NDAYIRAGIJE APANIA REKODI KUBWA

admin July 12, 2019 9:20 am


Kocha Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije, amesema, anachokifanya kwenye michuano ya Kagame nchini Rwanda ni kusaka rekodi ikiwemo kutetea kombe lao hilo.

Azam FC ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambayo mwaka huu inafanyika Rwanda, Jumapili iliyopita ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Idd Seleman ‘Nado’ dhidi ya Mukure FC ambapo jana walishuka dimbani kuvaana na KCCA ya Uganda.

Ndayiragije raia wa Burundi, huu ni msimu wake wa kwanza ndani ya Azam FC baada ya kujiunga nayo akitokea KMC. 

Ndayiragije amesema anataka aweke rekodi akiwa na Azam FC ya kuchukua Kombe la Kagame kwa mara ya tatu ili ajitengenezee njia ya kuelekea kulitwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu ujao.

“Kila kocha anahitaji rekodi kwenye kila timu, hivyo mimi nataka niiwezeshe Azam FC kutwaa Kombe la Kagame kwa mara ya tatu mfululizo, ambapo naamini hiyo itanipa nguvu ya kuliwania Kombe la Ligi Kuu Bara msimu ujao,” alisema Ndayiragije.

YANGA NAYO YATUMA MAJINA 26 CAF TAYARI KUKIIGA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YUMO SHIKALO AJIBU, GADIEL WAPELEKWA MAMELODI SUNDOWNS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply