KYLIAN Mbappe mshambuliaji wa PSG amewekewa ngumu na uongozi wa kikosi hicho kutimka ndani ya kikosi hicho kutokana na mkataba wake kumtaka aendelee kubaki ndani ya PSG.
Mbappe anahusishwa kujiunga na Real Madrid na sababu ikielezwa kwamba anataka kuchezeshwa kama mshambuliaji wa kati ambapo kwa sasa anachezeshwa Edinson Cavan na yeye akichezeshwa kama winga.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimeeleza kwamba Mbappe ana kandarasi ya miaka mitatu hivyo ishu ya kuondoka kwake kikosini hapo itakuwa ngumu labda alazimishe yeye kusepa.
SOMA NA HII HUYU HAPA KOCHA BORA WA MWEZI JANUARI, MZUNGU WA SIMBA NA MALALE HAMSINI WAPIGWA KIKUMBO