Uncategorized

ZAHERA AMPA YONDANI KITAMBAA CHA AJIBU

admin July 13, 2019 9:35 pm


Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga yupo mbioni kumrejeshea kitambaa cha unahodha beki Kelvin Yonddani.

Hatua hii imekuja mara baada ya aliyekabidhiwa kitambaa hicho, Ibrahim Ajibu kutimkia Simba ambako amesaini mkataba wa miaka miwili.

Taarifa zinasema Zahera ameamua kufikiria kumrejeshea tena Yondan baada ya kumpoka siku za hivi karibuni kutokana na makosa ya kinidhamu.

Yondani ambaye pia aliwahi kuichezea Simba sasa kuna dalili kubwa za kuendelea kuvaa kitambaa hicho.

Beki huyo mkongwe wa Yanga na Taifa Stars atakuwa anashikilia kitambaa hicho kwa muda mrefu tangu akichukue kutoka kwa kaka yake Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye amestaafu soka.

UKURASA WA MBELE WA GAZETI LA SPOTI XTRA LEO JUMAPILI, HUKO SIMBA KUMENOGA AZAM FC: ROBO FAINALI SI MCHEZO, TUTAPAMBANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply