Uncategorized

ORIGI MCHAWI WA MABAO YA USIKU NDANI YA LIVERPOOL FURAHA KAMA YOTE

admin July 14, 2019 8:05 am
DIVOCK Origi ambaye tangu ajiunge na Liverpool inayotumia uwanja wa Anfield tangu mwaka 2014 akitokea kikosi cha Lille amekuwa ni mtu mwenye furaha muda wote na amesema kuwa hafikirii kuondoka ndani ya kikosi hicho.
Origi ambaye ameongeza mkataba ndani ya kikosi hicho hivi karibuni na mabosi hao wakagoma kueleza muda wa mkataba wake zaidi ya kueleza kwamba ni mkataba mrefu amesema anafurahia maisha ya ndani ya kikosi hicho.
Raia huyo wa Ubelgiji anarekodi ya kufunga mabao mengi ya usiku na kumbuku zinaonyesha kwamba alifunga moja ya bao muhimu kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Barcelona kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Amefunga jumla ya mabao 28 kwenye michezo 97 ambayo amecheza mpaka sasa ndani ya kikosi hicho.
 “Nafurahi kuwa ndani ya kikosi hiki nina amini nitaendelea kufanya vema kila wakati,” amesema.
ZINEDINE ZIDANE AIKACHA KAMBI KUTOKANA MATIZO YA KIFAMILIA LIONEL MESSI ANABALAA KWENYE SUALA LA POCHI NENE, CR 7 HAONI NDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply