Home Uncategorized POLISI TANZANIA YABAKISHA WAWILI TU KWA SASA

POLISI TANZANIA YABAKISHA WAWILI TU KWA SASA

0


SELEMAN Matola Kocha wa Polisi Tanzania amesema kuwa bado wachezaji wawili ili akamilishe kukisuka kikosi chake kipya.

Matola amesema kuwa hadi sasa amesajili wachezaji 11 kati ya 13 aliokuwa anawahitaji kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

“Nahitaji kuwa na kikosi imara na kitakacholeta ushindani msimu ujao, kwa sasa zimebaki nafasi mbili tu ili kukamilisha usajili,” amesema.