Uncategorized

MABINGWA WA AFRIKA ALGERIA WANATISHA KINOMA

admin July 20, 2019 9:01 am


ALGERIA mabingwa wapya wa Afrika wanatisha kwani licha ya wapinzani wao Senegal kutawala mchezo kwa kupiga jumla ya pasi 320 huku wao wakipiga jumla ya pasi 201 bado walilinda bao lao.

Bao la mabingwa hao lilifungwa kwa shuti kali lililopigwa na Bagdad Bounebdjah na lilimgonga beki wa Senegal, Cheikhou Kouyate kabla ya kuzama nyavuni.

Jitihada za mshambuliaji Sadio Mane hazikuzaa matunda kwani licha ya kupambana na kuiongoza safu yake ya ushambuliaji kupiga jumla ya mashuti 11 langoni huku mabingwa hao wakipiga shuti moja hakuna kilichobadilika.

Algeria wanaingia kwenye orodha ya timu zilizotwaa ubingwa huo mara mbili huku Senegal wakiingia kwenye rekodi ya timu zilizoingia kwenye fainali ya michuano hiyo mikubwa mara mbili.

NAMUNGO FC, MTIBWA SUGAR, MBAO FC ZAINGIA ANGA ZA MWADUI FC KCCA WAAMBIWA NA AZAM FC DAWA YAO ISHAPATIKANA KESHO WANAKALISHWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply