NYOTA wa timu ya Taifa ya Senegal, Sadio Mane amesema kuwa kilichowaponza washindwe kutwaa kombe la Afcon mwaka 2019 ni kushindwa kutumia nafasi walizozipata.
Senegal imetinga hatua ya fainali ya michuano ya Afrika mara mbili na imeambulia patupu muda wote.
Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2002 na ilifungwa na Cameroon kwa penalti nchini Mali na fainali yake ya pili ikafungwa na Algeria bao la mapema kabisa dakika ya pili nchini Misri.
Mane amesema kuwa kilichowaponza washindwe kupata ushindi ni kushindwa kutumia nafasi walizozipata jambo lililowafelisha.
“Tumeshindwa kutwaa kombe kutokana na kushindwa kutumia nafasi tulizozipata, wenzetu mapema walitumia nafasi waliyoipata hapo ndipo tulipokwama na inaumiza kweli,” amesema.
Algeria mara ya mwisho kutwaa taji hilo ilikuwa ni mwaka 1990 na wamelitwaa tena mwaka 2019 baada ya kupita miaka 29.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.