KUMEKUCHA kimatafa ambapo mabingwa wa kombe la Shirikisho Azam FC, itaenyana na Fasil Kenema ya Ethiopia kwenye raundi ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo wa kwanza itakuwa ugenini kwenye mji wa Gondar, Ethiopia kati ya Agosti 9-11, huku ikimaliza kazi katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kati ya Agosti 23-25 mwaka huu.
Kama Azam FC itapenya kwenye raundi ya kwanza watakutana na mshindi wa jumla wa mechi kati ya Triangle FC ya Zimbabwe na Rukinzo ya Burundi, ikianzia nyumbani kati ya Septemba 13-15 kabla ya kurudiana ugenini Septemba 27-29, mwaka huu.
Ikitokea wakatusua kiunzi hicho basi watakuwa wamebakisha raundi ya mwisho ya mtoano kabla ya kuingia hatua ya makundi, na hapo itatarajia kucheza na moja ya timu zilizotolewa kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.