Uncategorized

KMC USOKWAUSO NA HARUNA NIYONZIMA WA SIMBA

admin July 25, 2019 1:31 am


UONGOZI wa KMC umesema kuwa hawana hofu na timu ya AS Kigali ambayo nyota wa zamani wa Simba Haruna Niyonzima amesajiliwa msimu huu.

KMC itamenyana na AS Kigali kwenye mchezo wa awali wa michuano ya Shirikisho nchini Rwanda kabla ya kurudiana Dar.

Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa wameanza maandalizi mapema yatakayoimarisha kikosi chao kiwe cha ushindani.

“Tumeanza kujiaanda kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya AS Kigali na matumaini yetu ni kupeperusha vema Bendera ya Taifa hivyo mashabiki watupe sapoti kwani tupo tayari,” amesema.

Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 9-11 na marudiano yaatarajiwa kuwa kati ya Agosti 23-25.

NYOTA SABA KUJIUNGA LEO NA TIMU YA TAIFA, MMOJA TAARIFA ZAKE HAZIFAHAMIKI AZAM FC YAWAITA MASHABIKI KUIPASAPOTI KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply