Uncategorized

NDAYIRAGIJE:KIKOSI KIPO TAYARI KWA USHINDI LEO

admin July 28, 2019 5:40 am

ETTIENE Ndayiragije, Kaimu Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa kazi leo ni moja kupata matokeo chanya mbele ya Kenya ili kufuzu michuano ya Chan.

Stars leo inamenyana na Kenya uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 kwa ajili ya kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Chan itakayofanyika mwaka 2020 nchini Cameroon.

“Kazi yetu leo ni moja tu kupata matokeo chanya yatakayotupa nafasi ya kusonga mbele kwani hatuna chaguo lingine.

“Kikosi kipo sawa na wachezaji tumewaandaa kisaikolojia na kiakili kuweza kupambana, tupo nyumbani ni lazima tutumie vema uwanja wa nyumbani mashabiki watupe sapoti,” amesema.

MWANAMICHEZO AZIM DEWJI AZIDI KUTENGAMAA FIFA KUMPA TUZO YA HESHIMA NYOTA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply