Uncategorized

YANGA YATUMIA MILIONI KUBORESHA HOSPITALI YA MWANANYAMALA

admin July 28, 2019 10:31 pm

TAWI la nguvu ya Buku la Yanga lenye makazi yake Mwananyamala jana limekabidhi msaada wa ukarabati wa Wodi ya Wanaume no.5 waliokuwa wakifanya kwa takribani wiki moja kuelekea kilele cha siku ya Wananchi Agosti 4,2019.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Mussa Wambura amesema:- “Kitendo mlichokifanya kitabaki kuwa historia kwa Hospitali ya Mwanabyamala na kuwaomba jamii ziige kutoa misaada ya namna hii inayomgusa kila binadamu kwani Hospitali ni yetu sote tusiiachie Serikali tu, jukumu hili ni la kila mmoja,”.
 Mwenyekiti wa Nguvu ya Buku, Ally Kuacha amewapongeza wanachama wake kwa kujitoa mpaka kukamilisha mchakato mzima waliokuwa wamekusudia kuelekea kilele cha siku ya Wananchi na kuwaomba waendelee na mshikamano.

 Katibu wa Tawi la Yanga la Nguvu ya Buku, Juma Iyagala amesema ukarabati huo wa Wodi ya Wanaume umegharimu Shilingi 1,830,000/= ambao ni kupaka rangi ndani na nje, kupaka rangi bati pamoja na kubadilisha nyavu za mbu.

YANGA WACHEKELEA UJIO WA ZAHERA,, MBELGIJI AIPA YANGA SIRI ZA USHINDI, KESHO CHAMPIONI JUMATATU LIVERPOOL: TUNA MECHI NYINGI MSIMU UJAO LAZIMA TUFANYE KWELI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply