Uncategorized

LUKAKU NAYE YUPO NJIA PANDA, ATAKA KUTIMKIA ITALIA

admin August 2, 2019 7:22 am

ROMELU Lukaku, mshambuliaji wa Manchester United amesema kuwa kwa sasa anafikiria kutua timu moja wapo ambayo inashiriki Serie A kati ya Juventus ama Inter Milan.

Kaka yake na Lukaku, Jordan amejiunga na Lazio mwaka 2016 jambo ambalo linatajwa kuwa sababu ya yeye kutaka kujiunga huko na amekuwa akijifunza lugha ya kiitaliano.

Lukaku amesema: “Kaka yangu anacheza Italia, nimekuwa nikitazama michezo yake mingi nimependa namna ilivyo na wanavyozungumza.

Inter Milan walikuwa mstari wa mbele kuipata saini yake ila inaelezwa dili lilibuma na sasa anazungumza na Juventus.

Juventus wapo tayari kumuacha Paulo Dybala kwenda Manchester United ndani ya Uwanja wa Old Trafford kama sehemu ya dili la Lukaku.

United imesema thamani ya Lukaku ni pauni Milioni 75 na hawapo tayari kushusha dau hilo.

KOCHA TIMU YA TAIFA: HAKUNA NAMNA LAZIMA WAPIGWE TU LEO WAPINZANI WETU SIMBA: TUTAWAFURAHISHA MASHABIKI KWENYE KILA MCHEZO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply