Uncategorized

KOCHA TIMU YA TAIFA: HAKUNA NAMNA LAZIMA WAPIGWE TU LEO WAPINZANI WETU

admin August 2, 2019 6:32 am

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ amesema leo hakuna namna lazima wawachape wapinzani wao Botswana.

Tanzanite ipo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya COSAFA ambayo imeanza kutimua vumbi jana, leo wanakipiga mchezo wao wa kwanza na Botswana.

“Watanzania wanapaswa kuwa na imani na sisi, tumekuja kufanya kazi na tupo tayari kwa ushindani, morali waliyonayo wacheaji ni kubwa ni jambo la kusubiri wakati tu, lazima tupate matokeo chanya” amesema.

Mchezo wa leo dhidi ya Botswana utachezwa  Uwanja wa Gelvandale,Port Elizabeth,Afrika Kusini.

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA IJUMAA IJUMAA LUKAKU NAYE YUPO NJIA PANDA, ATAKA KUTIMKIA ITALIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply