RIPOTI zinaeleza kuwa, Paulo Dybala mshambuliaji wa Juventus amewaambia mabosi wake kuwa hana mpango wa kujiunga na Manchester United kwa kuhofia kumuweka kwenye hatari Romelu Lukaku.
Timu hizo mbili pamoja na wakala wa Lukaku zipo kwenye mazungumzo ya kubadilishana wachezaji hao na anayesuburiwa ni Dybala mwenyewe kukamilisha dili hilo.
Alhamisi iliyopita alirejea Turin na hatarajiwi kujiunga na Juventus Jumatatu na wala hajaonana na Meneja Maurizio Sarri.
Licha ya kuambiwa na nyota wa zamani wa Manchester United ambaye anakipiga Juventus kwa sasa, Cristiano Ronaldo kwamba Manchester United ni sehemu salama kwake kwani wanaweza kuwa Mabingwa amechomoa ushauri huo.
Dybla aliomba ushauri kupitia kundi la WhatsApp la wachezaji juu ya kwenda kwake Old Trafford ambapo atabadilishana na Lukaku na Ronaldo akamwambia ni bora akijiunga na klabu hiyo.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.