Uncategorized

MORGAN GIGGS-WHITES KINDA WA WOLVES ANAYETUMAINIWA KUFANYA MAAJABU

admin August 7, 2019 6:07 pm

KIUNGO wa Wolves, Morgan Gibbs-Whites msimu uliopita alikuwa kwenye maandalizi kwa ajili ya msimu ujao unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 9.
Kinda huyo anayekipiga Wolves ana umri wa miaka 19 tu na ameshaanza kupata uzoefu wa kucheza mechi kubwa na ngumu ndani ya Premier League.
Msimu uliopita alicheza jumla ya mechi 26 na ameanza kwenye jumla ya mechi saba ambazo zote alizimaliza na alikuwa anahusika kwenye maandalizi ya mechi za Ligi ya Europa.
Ni zao la timu ya vijana ya Wolves ambayo imemkuza na kumfanya awe na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kutoa pasi zenye uhakika kwa nafasi ambayo anaicheza kwa sasa.
Ameongeza ujasiri na uwezo baada ya kuaza kwenye mchezo wa maandalizi ya msimu ujao dhidi ya Newcasstle United ambapo alipata bahati ya kufunga bao.
YANGA YAINGIA ANGA ZA SIMBA ISHU YA MAVAZI SportPesa, SIMBA YATOA VIFAA KWA MICHEZO KWA TIMU TATU BONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply