Home Uncategorized SIMBA YAWAZUIA MASHABIKI KUIZOMEA YANGA, HAYA NDIO MAAMUZI YA UONGOZI KIMATAIFA

SIMBA YAWAZUIA MASHABIKI KUIZOMEA YANGA, HAYA NDIO MAAMUZI YA UONGOZI KIMATAIFA


KUELEKEA kwenye michezo ya kiamataifa ambayo inatarajia kuanza kesho kwa timu nne za Tanzania kupeperusha Bendera ya Kimataifa, Uongozi wa Simba umewazuia mashabiki wa Simba kuzomea wawakilishi wa Taifa.

Simba na Yanga zimekuwa na utamaduni wao hasa inapofika suala la kushangilia kimataifa ambapo imekuwa kawaida kwa timu moja kshabikia wapinzani jambo ambalo uongozi wa Simba umelikemea.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa: “Imetuchukua miongo kadhaa kama nchi kupata fursa ya kuwakilishwa na vilabu vinne kwenye mashindano ya CAF,
Na Simba ina mchango katika hili.


“Kama Taifa tunatakiwa tufanye vizuri zaidi kupitia wawakilishi wetu ili tuendelee kwa miaka ijayo kuwa na klabu nne katika CAF Competitions (michuano ya Caf).


“Najua ni ngumu kunielewa leo lakini nawaomba Wanasimba wote kesho msizomee Yanga, msilipe kisasi na wekeni maslahi mapana ya nchi, sisi ni waungwana na uungwana ni vitendo.

“Kama hujiwezi usiende Taifa na ikibidi kwenda na huwezi kuwashangilia bora ukae kimya.Najua walitukera msimu uliopita lakini tuiangalie nchi kwanza na pia tujue wao,Azam na KMC pamoja na sisi ndio tuna nafasi ya kuendelea kupewa nafasi nne tena msimu ujao.

“Naiangalia Tanzania kama nchi,utani na kuzodoana kwetu utatugharimu sote,kama kuwacheka tuwacheke baadae lakini kwa sasa interest (maslahi) ya Tanzania iwe moja,” amesema.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA