Home Uncategorized TATIZO LA YANGA KIMATAIFA LIPO HAPA, WAPANIA KUWAPOTEZA TOWNSHIP ROLLERS KESHO

TATIZO LA YANGA KIMATAIFA LIPO HAPA, WAPANIA KUWAPOTEZA TOWNSHIP ROLLERS KESHO


BAADA ya Jana Yanga kukamilisha ratiba ya michezo yake miwili visiwani Zanzibar leo wanatarajia kurejea Bongo.

Kwenye kambi ndogo visiwani Zanzibar ilicheza mechi mbili ambazo ni pamoja na ile dhidi ya Mlandege FC ambapo ilishinda kwa mabao 4-1 na mchezo wa mwisho ulikuwa dhidi ya Malindi FC.

Mchezo wa mwisho Yanga ililazimisha Sare ya kufungana bao 1-1 visiwani humo huku wao wakianza kufunga dakika ya 16 kupitia kwa Deus Kaseke kabla ya Malindi kusawazisha dakika ya 90.

Mwinyi Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anaona kikosi kinaimarika licha ya changamoto ndogondogo. 


“Tupo Sawa tatizo kubwa ni kwenye muunganiko, ila ninaamini tutafanya vema kitaifa na kimataifa, wachezaji wengi walikuwa wametofautiana muda wa kuanza mazoezi ila kazi naona ni nzuri”. 

Kesho Yanga itakuwa Uwanja wa Taifa ikimenyana na Township Rollers, mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  UMAKINI NA TAHADHARI KWA SASA NI MUHIMU