Uncategorized

YANGA WAIPA SAPOTI SIMBA KIMATAIFA, WAPANIA KUWAKALISHA ROLLERS LEO TAIFA

admin August 10, 2019 11:59 am


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utatoa sapoti kwa timu zote ambazo zinashiriki michuano ya kimataifa Afrika inayoandaliwa na Caf ikiwa ni pamoja na Simba.

Timu hizo ambazo ni pamoja na watani wao Simba leo watamenyana na UD do Songo ya Msumbiji, KMC wao watamenyana na  AS Kigali ya Rwanda huku Azam FC wao kesho watamenyana na Fasil Kenema ya Ethiopia.

Kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram Yanga wameandika namna hii:”Safari ya Kimataifa imeshaanza dude linaamka leo pale uwanja wa Taifa, Township Rollers wanaenda kukaa.

“Tanzania ni nchi yenye Umoja na Mshikamano, hivyo hatutaruhusu kirahisi timu yetu yoyote ya nyumbani ipoteze point 3 dhidi ya timu ya nje.

 “Tutasapoti Taifa Letu na Timu zetu zote za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya CAF.

“Ajabu itakua wewe Mwananchi na Mzalendo kubaki nyumbani.

“Uzuri bei ni za wananchi.Viingilio kwa Mzunguko ni Tsh 5,000 VIP B na C Tsh 15,000 tu. Na VIP utakaa kwa Tshs. 50,000 tu,”. 

LUKAKU AMUACHIA JEZI MARTIAL NDANI YA UNITED KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA UD do SONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply