Uncategorized

JKT WAIKACHA BONGO, WATIMKIA VISIWANI HUKO KWENYE UPEPO

admin August 12, 2019 9:31 pm


KIKOSI cha JKT Tanzania kimejichimbia Visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza kutimu vumbi Agosti 23.

JKT Tanzania mchezo wake wa kwanza itamenyana na Simba, Agosti 23 uwanja wa Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Abdalah Mohamed ‘Bares’ amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na hesabu ni kufanya vema.

“Kikosi kipo salama na wachezaji wana morali, hivyo kufanya vema ndio mpango wetu mkubwa kwenye ligi kuu Bara.

“Sapoti kwa mashabiki na wadau kwani tunaamini ligi itakuwa na ushindani mkubwa ila tupo tayari,” amesema.

TANZANITE YAREJEA KIBABE, MBALI NA KOMBE WAMEBEBA TUZO NNE KUMBE! ROLLERS YAIPELEKA YANGA KILIMANJARO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply